Udhaifu wa dai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur-an ili kuwania Madaraka na ukubwa.

Udhaifu wa dai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur-an ili kuwania Madaraka na ukubwa.

 

Add Comment
 • 1 Answer(s)

  Fikra za kuwa Muhammad (s.a.w)  aliitunga Qur-an kwa sababu aliwania ukubwa na madaraka pia ni vigumu kuithibitisha, kwa sababu zifuatazo:

  1.Muhammad (s.a.w) alijulikna sana ulimwengu mzima kama kiongozi aliyefanikiwa sana katika historia ya banaadamu. Mtu mwenye sifa kama hizo angeweza kuchukua uongozi  na madaraka bila hatakudai kwanza Utume.  Kwa kufanya hivyo kungekuwa rahisi zaidi kwakwe kama alikuiwa anataka madaraka kuliko kudai Utume kwanza.

  2.Qur-an imetamka waziwazi kuwa hakuna mtu yoyote ikiwa ni pamoja na Muhammad (s.a.w) mwenyewe awezae kuleta mfano wake. Kama lengo lake ilikuwa kupata utukufu miongoni mwa watu angejitapa kuwa ndiye mtunzi wa kitabu hikikinachovishinda vitabu vyote. Wakati  Fulani waislamu walikuwa wanasimama walipotaka kumuamkia kama ishara ya heshima, lakini aliwakataza na kuwaambia “Msisimame kama waajami wanavyofanya, baadhi yao kuwatukuza wengine”

  3.Hisia za Muhammad (s.a.w) baada ya kupata wahy mwanzo zinaonyesha kuwa hakuwa anawania ukubwa kisiri siri. Baadaya yaliyomtokea katika pango la Hira alirejea haraka kwa mkewe hali ya kuwa anatetemeka kwa hofu kama kwamba alikuwa na homa kali, akamuomba mkewe amfunike nguo nzito. Baada ya hofu kumuondoka akamsimulia mkewe yote aliyoyaona kisah akasema,”Ewe Khadija, ni lipi linataka kunisibu?” ni dhahiri kuwa kama kusingizia kupata wahy ilikuwa ni mbinu tu ya kujipatia ukubwa Muhammad (s.a.w) asingehofia chochote. (Qur’an 28:86).

  Premier Answered on March 3, 2019.
  Add Comment

  Your Answer

  By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.