Taja tofauti kati ya Fasihi Andishi na Fasihi Simulizi

Premier Asked on September 19, 2019 in Kiswahili.
Add Comment
 • 1 Answer(s)
  FASIHI SIMULIZI FASIHI ANDISHI
  1. Huwasilishwa kwa njia ya mdomo na/au matendo. Huwasilishwa kwa njia ya maandishi
  2. Fasihi simulizi ni mali ya jamii. Kazi andishi ni mali ya mwandishi (na mchapishaji)
  3. Msimulizi anaweza kubadilisha sehemu fulani

   

  Kitabu kilichoandikwa hakiwezi kubadilishwa
  4. Huhifadhiwa na kurisishwa kizazi hadi kizazi (akilini). Huhifadhiwa vitabuni
  5. Kazi simulizi hubadilika na wakati Kazi andishi haibadiliki na wakati
  6. Huhitaji msimulizi na hadhira yake wawe mahali pamoja wakati wa masimulizi Msomaji anaweza kusoma kitabu cha hadithi peke yake, mahali popote, wakati wowote
  7. Mtu yeyote anaweza kutunga na kusimulia Ni lazima mwandishi na msomaji wawe na uwezo wa kusoma
  8. Hutumia wahusika changamano (wanyama, watu, mazimwi n.k) Hutumia wahusika wanadamu
  Premier Answered on September 19, 2019.
  Add Comment

  Your Answer

  By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.