Taja njia za kuondoa utata katika Lugha ya Kiswahili

Elezea njia tofauti za kuondosha utata katika Lugha ya Kiswahili

Premier Asked on September 19, 2019 in Kiswahili.
Add Comment
 • 1 Answer(s)

  Tungo tata ni tungo ambazo huwa na maana zaidi ya moja ndani yake. Mara nyingi utata katika lugha ya kiswahili hujitokeza katika maandishi kuliko kwenye mazungumzo kwa sababu mazungumzo huzingatia zaidi mazingira ya wazungumzaji na wakati. Zifuatazo njia mbalimbali zinazo tumika katika kuondosha utata katika lugha ya kiswahili:-

  (1) Kutoa maana zaidi kwa yale maneno yenye maana zaidi ya moja na kuongeza viambishi ili kubainisha maana iliokusudiwa. Kwa  Mfano Mbuzi wake ameibiwa au Mbuzi wake wameibiwa

  (2) Kuzingatia kanuni za uandishi hasa ni matumizi na alama na vituo tunapoandika. Mfano   (i) Mama latifa yupo? (ii) Mama, latifa yupo. (iii) Mama, latifa yupo? (iv) Mama latifa yupo.

  (3) Kuzingatia matumizi sahihi katika mazingira muafaka ya vinganishi  na vihusishi. Kwa Mfano Ali anakula wali kwa kuku baala ya  Ali anakula wali na kuku

  (4) Tueke shada au mkwazo kwa yale maneno yanayohitaji hali hiyo, ili kupata maana iliyokusudiwa. Kwa mfano Ali ameonekana barabara

  (5) Tuyaepuke matumizi mabaya ya fasihi, kwa sehemu zisizo hitajika yaani tutmie lugha ya kawaida. Kwa Mfano Baada ya kusema Ali amevaa miwani basi tuseme Ali amelewa.

  (6) Tueke bayana matumizi ya vitendo kwa kutoa maelezo zaidi kwa vile vitendo vinavyotoa maana zaidi ya moja tunapotumia katika tungo. Kwa mfano Baada ya kusema mtoto wake ameibiwa basi tuseme Vitu vya mtoto  wake vimeibiwa.

  Premier Answered on September 19, 2019.
  Add Comment

  Your Answer

  By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.