Orodhesha mambo saba yanayo onesha umuhimu wa kusimamisha swala kwa mujibu wa qur-an na sunna?

Mambo saba yanayo onesha umuhimu wa kusimamisha swala kwa mujibu wa qur-an na sunna.

Add Comment
 • 1 Answer(s)

  Kusimamishwa swala ni kuswali kwa kutekeleza kwa ukamilifu sharti zote za swala, nguzo zote za swala, kuwa na khushui (unyenyekevu) wakati wa kutekeleza masharti ya swala na wakati wa kuswali kuanzia mwanzo wa swala mpaka mwisho wa swala na kudumu na swala mpaka mwisho wa uhai.Kusimamishwa swala kumesisitizwa sana katika Uislamu kwa sababu zifuatazo:

  1.Kusimamisha swala ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w), Amri ya kusimamisha swala imesisitizwa katika aya mbalimbali za Qur-an, (Qur-an “29:45”, “4:103”, “14:31”)

  2.Kusimamisha swala ni nguzo ya Uislamu, Kusimamisha swalani nguzo ya pili ya Uislamu baada ya shahada kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo,

  ”Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema “Uislamu umjengwa juu ya nguzo tano, kushuhudia kuwa hapana Mola ila Mwenyezi Mungu na kushuhudia kuwa Muhammad ni mtume wa Mwenyezi Mungu, kusimamisha swala, kutoa zakat, kufunga ramadhani na kuhiji nyumba takatifu (Al-kaaba) kwa mwenye uwezo” (Bukhari na Muslim).

  3. Kusimamisha swala ndiyo kitambulisho cha Muislamu, Amesimulia Jabir (r.a) kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema “Tofauti kati ya mja na kafiri ni kuacha swala”. Muslim.

  Biraidah (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema, “Tofauiti iliyopo kati yetu na wao ni mwenye kuacha swala, Mwenye kuacha swala si Muumini (ni kafiri)” (Ahmad, Abu Daudi, AN-Nasai, Tirmidh, Ibn Majah).

  4. Swala ni ufunhguo wa peponi, Katika hadithi aliyosimulia Jabir bin Abdillah(r.a) Mtume (s.a.w) amesema: “Ufunguo wa peponi ni swala na ufunguo wa swala ni tohara” (Muslim).

  5. Swala ndio amali ya kwanza kuhesabiwa siku ya Hesabu, Abuu Huraira (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema Amali ya kwanza atakayo ulizwa mja siku ya kiama (siku ya hukumu) ni swala. Swala zake zikiwa zimekamilika atafuzu, na kama swala zake zitakuwa pungufu atafeli na kuhasirika. Kama swala zake za faradhi zitakuwa zimepungua, Mwenyezi Mungu mtukufu wa daraja atasema ‘Angalia kwa mja wangu kama ana swala za ziada (swala za sunna) ili zichukuliwe kujazia sehemu iliyopungua katika swala za faradhi. Kisah ndio vitendo vyake vingine vitaangaliwa kwa namna hiyo hiyo” (Tirmidh, Abu Daud, An-Nasai, Ibn Majah na Ahmad).

  Premier Answered on April 28, 2019.
  Add Comment

  Your Answer

  By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.