Nini maana ya Visasili?

Visasili ni hadithi zinazohusu mianzo ya maumbile, tabia au matendo fulani. Mathalan mianzo ya matendo kama vile ndoa, tohara na imani mbalimbali. Mara nyingi visasili hutumiwa katika lugha ya kimafumbo.

Sifa za visa asili

 1. Huwa na mianzo na miishio maalum, kwa mfano, Hapo zamani za kale..
 2. Hueleza matukio ya jadi kwa mfano, asili ya watu, kitu, kufanya kazi, kula na kadhalika.
 3.  Hueleza imani pamoja na desturi za jamii. Huelezea misimu, miungu yenye uwezo mkubwa wa kusababisha mambo na uliopita wa binadamu.
 4.  Huchukuliwa na jamii husika kuwa ni kweli.
 5. Mandhari ya visa asili huwa si ya kawaida kwa mfano, madhari ya milima .
 6.  Wahusika huwa na aina mbali mbali kwa mfano, binadamu wanyama au hata miungu.
 7. Wahusika huwa bapa; hawabadiliki

 

Premier Asked on August 29, 2018 in Kiswahili.
Add Comment
 • 0 Answer(s)

  Your Answer

  By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.