kwa kutumia ushahidi wa qur-an thibitisha kuwa suala la kuwepo siku ya malipo ni jambo linalowezekana?

kwa kutumia ushahidi wa quran thibitisha kuwa suala la kuwepo siku ya malipo ni jambo linalowezekana?

Add Comment
 • 1 Answer(s)

  Kuamini siku ya mwisho (siku ya malipo) ni nguza ya tano ya imani ya kiislamu, pamoja na nguzo hii kuwa ya tano kaika orodha ya nguzo za imani ni nguzo ya msingi mno kwani ndio nguzo inayompa mja msukumo wa kutenda wema na kujiepusha na maovu katika maisha ya kila siku kwa matarajio ya kupata makazi mema ya pepomi na kuepukana na adhabu kali ya motoni.

  Kuamini siku ya malipo ni miongozi mwa mambo ya ghaibu ambayo mwanaadamu hana uwezo wa kuyadiriki kwa milango yafahamu bali huhitajia matumizi makubwa ya akili pamoja na elimu ya ufunuo (Wahyi) kutoka kwa Allah (s.w) kupitia kwa Mitume wake. Mitume walifahamishwa vyema mazingira halisi ya siku ya mwisho ,iloi waweaze kuwaonya na kuwatahadharisha wanaadamu kwa maisha hayo kwa msisitizo wa uhakika. Kimantiki lazima kuwepo na siku ya malipo kwa sababu zifuatazi:-

  1.Mwanaadamu aulizwe juu ya vipaji na neema mbalimbali alizotunukiwa na mola wake alitumiaje, Pamoja na elimu yote aliyotunukiwa binaadamu bado amepewa uhuru wa kuamua juu ya kuamini Mwenyezi Mungu na kumuabudu inavyostahili au kumkana Mwenyezi Mungu na kuwaabudu wengine badala yake,Kimantiki ni lazima pawe na siku ya malipo, ili mwanaadamu aulizwe jinsi alivyozitumia neema za Mwenyezi Mungu (s.w) na vipaji alivyotunukiwa katika kuendea lengo la kuumbwa kwakwe (Qur-an 102:8).

  2.Mfumo au njia sahihi ya maisha ibainishwe, Kimantiki hatuna budi kukubali kuwa njia ya maisha iliyo sahihi ni lazima iwe mija tu kwasababu mwanaadamu ni jamii moja yenye lengo moja la maisha na wenye usawa katika kuhitaji mahitaji muhimu yanayowafanya waishi kwa furaha na amani.

  Kimantiki njia hii ni lazima ifundishwa au ielekezwe na Muumba wa mwanaadamu, hivi ndivyo hasa alivyofanya Muumba kwa kuleta mitume na vitabu vya kuelekeza njia hiyo, Lakini pamoja na kuletewa mwongozo kwa njia ya Mitume na vitabu, bado wanaadamu wamepewa uhuru wa kufuata mwongo huu wakiamua kufanya hivyo au kuukanusha na kufuata miongozo mengine waliyoiunda wao wenyewe. Hivyo ni lazima iwepo siku ya mwisho ili ibainike dini au njia sahihi ya maisha (Qur-an 16:39).

  3.Ubainike ukweli kwa waliozuliwa uovu, Pamoja na ulazima wakubainishwa tofauti kati ya njia za maisha, pia kuna ulazima wa kuwa na siku ya kubainishwa haki kati ya watu binafsi au vikundi vya watu. Mtu binafsi au kikundi cha watu waweza kusingiziwa jambo na pakatolewa ushahidi wa uongo kwa maslahi ya mtu au kikudni Fulani mpaka ikawa vigumu kwa walimwengu kuona ukweli kinyume na shutuma. Ni lazima pawe na siku ambayo ukweli utabainishwa na mjjuzi wa mambo yote, ndio mana tunaposingiziwa jambo tunamtupia Mwenyezi Mungu kwa viapo tukiwa na uhakika kabisa kuwa kuna siku tutakuwa mbele yake atatuamua kwa uadilifu.

  Premier Answered on April 28, 2019.
  Add Comment

  Your Answer

  By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.