Elezea maana ya Visa asili?

Visasili ni hadithi zinazohusu mianzo ya maumbile, tabia au matendo fulani. Mathalan mianzo ya matendo kama vile ndoa, tohara na imani mbalimbali. Mara nyingi visasili hutumiwa katika lugha ya kimafumbo. J.G. Frazer anasema visasili ni upangaji wa matukio kinathari ambapo hapo awali matukio haya yalihusishwa na matukio kama sherehe, uganga, uchawi na uramli. Ni hadithi inayobuniwa kueleza juu ya ada fulani ilivyoanza. Hivyo kisasili huwekea mantiki tukio la kiada,chanzo chake na jinsi lilivyopokelewa na vizazi mbalimbali katika jamii inayohusika.

Okpewho (1983) anadai kwamba asili ya kisasili hubadilika kulingana na mapito ya wakati kwa sababu ya usahaulifu wa watu wanaopaswa kukumbuka na vilevile kwa sababu ya mageuzi yanayoweza kutokea katika mazingira yao. Mabadiliko haya ni lazima yatatanishe toleo la kisasili cha asili. Tunaposonga nyuma katika mapito ya wakati uhakika wa kisasili hubainika zaidi.

Kisa cha mwanzo kina ukweli zaidi kikilinganishwa na kisa cha hivi karibuni zaidi ikiwa tendo linalosimuliwa katika kisasili fulani lilifanyika juzijuzi halina budi kuripotiwa kwa uaminifu zaidi kwa sababu washiriki katika tendo hilo watashadidia ushuhuda wa kweli kuhusu tendo hilo. Hivyo umbuji wa mtambaji huchangia ukweli au uzushi unaopatikana katika kisasili fulani. Kwa ujumla maoni ya wengi yanaafiki kuwa kisasili ni ukweli uliokolezwa na uzushi kama hamna uzushi hicho hakiwezi kuwa kisasili.

Premier Asked on February 17, 2018 in Kiswahili.
Add Comment
  • 0 Answer(s)

    Your Answer

    By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.