Bainisha hatua zilizo muhimu kwa wanandoa kuzifuata ili kuachana kiislamu?

Bainisha hatua zilizo muhimu kwa wanandoa kuzifuata ili kuachana kiislamu

 

Add Comment
 • 1 Answer(s)

  Talaka ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa waliofunga mume na mke wakati wa kufunga ndoa mbele ya mashahidi wawili. Baada ya kuvunja mkataba huu kwa kufuata sharia ya kiislamu, mwanamke aliyetalakiwa huwa huru kuolewa na mume mwengine. Zifuatazo ni hatua zilizo muhimu kwa wanandoa kuzifuata ili kuachana kiislamu:-

  1.Talaka hutolewa kwa matamshi aumaandishi kuwa “Nimekuacha” au kwa maneno mengine yenye maana hiyo.

  2.Utoaji wa talaka ushuhudiwe na mashahidi wawili waadilifu.

  3.Talaka itolewe wakati mke yup katika kipindi cha twahara na wasiwe wamefanya tendo la ndoa katika kipindi hiko (na kama wamefanya tendo la ndoa katika kipindi hicho cha twahara , talaka isitolewe kwani haitasihi.

  4.Baada ya talaka kutolewa mke analazimika kukaa edam le mle katika nyumba ya mumuewe wakiishi pamoja kama kawaida isipokuwa watatengana kwenye malazi. Kila mmoja atawajibika kwa mwenzake kama kawaida katika kipindi chote cha eda.

  Premier Answered on March 23, 2019.
  Add Comment

  Your Answer

  By posting your answer, you agree to the privacy policy and terms of service.