Ellimu Dini ya KiislamuNo Comments

Talaka ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa waliofunga mume na mke wakati wa kufunga ndoa mbele ya mashahidi wawili. Baada ya kuvunja mkataba huu kwa kufuata sharia ya kiislamu, mwanamke aliyetalakiwa huwa huru kuolewa na mume mwengine. Zifuatazo ni hatua zilizo muhimu kwa wanandoa kuzifuata ili kuachana kiislamu:-

1.Talaka hutolewa kwa matamshi aumaandishi kuwa “Nimekuacha” au kwa maneno mengine yenye maana hiyo.

2.Utoaji wa talaka ushuhudiwe na mashahidi wawili waadilifu.

3.Talaka itolewe wakati mke yupo katika kipindi cha twahara na wasiwe wamefanya tendo la ndoa katika kipindi hiko (na kama wamefanya tendo la ndoa katika kipindi hicho cha twahara , talaka isitolewe kwani haitasihi.

4.Baada ya talaka kutolewa mke analazimika kukaa eda mle mle katika nyumba ya mumuewe wakiishi pamoja kama kawaida isipokuwa watatengana kwenye malazi. Kila mmoja atawajibika kwa mwenzake kama kawaida katika kipindi chote cha eda.

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!