Ellimu Dini ya KiislamuNo Comments

Ndoa ni mkataba wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata utaratibu ulioweka na jamii.  Ndoa ya kiislamu ni mkataba wa hiari kati ya mume na mkewa kuishi pamoja kwa kuzingatia masharti na taratibu zilizowekwa na sharia ya kiislam. Ndoa yoyote iliyofungwa kinyume na masharti na taratibu za kiislam haikubaliki kwa waislam. Umuhimu wa ndoa kwa mtazamo wa Uislam :

1.Kuhifadhi jamii na zinaa; Mwenyezi Mungu (s.w) ameharamisha jimai nje ya ndoa ili kuikinga jamii na madhara makubwa ya zinaa ambayo huidunisha na kuivuruga jamii kwa kiasi kikubwa. Mwenyezi Mungu (s.w) amehalalisha ndoa na kuitilia mkwazo kwa wale wenye uwezo kama tunavyojifunza katika aya “4:24” na “5:5”.

2.Kuendeleza kizazai cha mwanaadamu kwa utaratibu mzuri; Lengo la ndoa haliishi kwenye kufanya jimai tu balikitendo hicho kinakusudiwa kiwe ndio sababu ya kupatikana watoto watakao endeleza kizazi cha mwanaadamu. Lengo hili la ndoa linabainishwa wazi katika aya (42:11) na (4:1).

3.Kujenga mapenzi, huruma na ushirikiano katika familia; Lengo jengine la ndoa ni kuleta utulivu wa moyo kati ya mumue na mke na kupandikiza mapenzi, huruma na ushirikiano kati yao na kuendeleza maadili hayo kwa watoto wao. Ushahidi wa lengo hili limebainishwa katika Qur-an (30:21) na ( 2:187).

4.Kukuza uhusiano na udugu katika jamii; Uhusiano na mshikamano wa kidamu wa familia moja hutanuka pale watoto wa familia moja watakapooana na watoto wa familia nyengine. Hivyo mapenzi, huruma na ushirikiano wa udugu hutanuka kutoka kwenye familia moja, kasha kwenye ukoo, kasha kwenye kabila hadi kufikia taifa na mataifa. Sisi sote tu familia ya Adam na Hawa , hivyo tunapaswa tupendane,tushirikiane na tuhurumiane kama tunavyokumbushwa katika Qur-an (49:13)

5.Kukilea kizazi katika maadili mema; Upendo kwa watoto hauishii tu kwenye kuwapa watoto chakula bali ni lazima uambatane na malezi yao yote. Malezi ya watoto ni pamoja na kuwaelimisha katika Nyanja mbalimbali zinazohusu maisha yao, kuwafunza tabia njema na utaratibu wa maisha anaouridhia Mwenyzi Mungu (s.w). Watoto waliokosa malezi ya kifamilia hata kama watapelekwe kwemye shule za malezi hawawezi kuwa sawa kitabia-upendo, huruma na mwnendo mwema na wae waliopata malezi ya familia.

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!