Ellimu Dini ya KiislamuNo Comments

1.Hawajui lengo la swala, Kutojua lengo la swala au kuipa swala lengo jengine lisilo lile alilobainisha Mwenyezi Mungu (s.w) ni sabau tosha ya kumfanya mwenye kusali asifikie lengo la swala. Lengo la swala kama ilivyobainishwa katika Qur-an …. “Hakika swala humzuiliya mtu na mambo machafu na maovu…”(29:45).

2.Hawahifadhi swala zao, Swala haimfikishi mja kwenye lengo lililokusidiwa na kutoa matunda yanayotarajiwa mpaka ihifadhiwe, Mwenyezi Mungu ametufahamisha kuwa “Wamefunzu waumin….na ambao swala zao huzihifadhi” (23:1,9)

Kuhifadhi swala ni kutekelezakwa ukamilifu sharti na nguzo zote za swala, Wengi wa waislamu wanaosalihawatekezlivilivyo sharti nanguzo za swala kwa kutojua au kwa kupuuza. Mbele ya Mwenyezi mungu ni kosa kubwa kupuuza swala au kufanya ibada kwa ujinga. Mwenyezi Mungu anakemea jambo hili katika qur-an (107:4-6)

3.Hawaswali kwa unyenyekevu, Unyenyekevu (khushui) ndio roho ya swala. Swala iliyosaliwa pasina unyenyekevu huwa si swala bali ni maiti ya swala. Ni wazi kwamba swala maiti haiwezi kumfikisha mja kwenye lengo lililokusudiwa.

Unyenyekevu katika swala hupatikana kwa kuwa na utulivu wamwili na fikra, na kuwa na mazingatio juu ya Mwenyezi Mungu (s.w). kumzingatia na kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndani ya swala ndio nguvu inayompelekeamwenye kuswali afikie lengo la swala kama qur-an inavyotufahamisha “(29:45).

 

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!