Ellimu Dini ya KiislamuNo Comments

Pamoja na kufanana katika baadhi ya sehemu kwa Qur-an na Biblia bado kimsingi, Qur-an na Biblia zimetofautiana kiasi kikubwa;-

1.Biblia si kitabu kimoja bali ni mkusanyiko wa vitabu 73 kwa mujibu wa madhehebu ya wakatoliki au vitabu 66 kwa mujibu wa madhehebu ya Waprotestanti. Vitabu jivyo viliandikwa na wananchi wasiopungua 40. Qur-an ni kitabu kimoja kilichotokea kwa Allah (s,w) na aya zake zote ziliandikwa mara tu bada ya kushuka.

2.Biblia ni kitabu chenye mchanganyiko wa maneno ya Mwenyezi Mungu,Mitume na maoni ya wanahistoria. Qur-an ni neno la Allah (s.w) tu peke yake. Hata maneno ya Muhhamad (s.a.w) hayamo katika Qur-an.

3.Katika Agano la Kale na Jipya yapo maelezo juuya historia ya maisha ya mitume. Kumbukumbu la torati siyo tu ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu bali pia historia ya maisha ya nabii Mussa (a.s) Injili ya Mathayo, Luka, Marko na Yohana zinaelezea historia ya Yesu kama ilivyosimuliwa na wanafunzi wake. Qur-an inatja ahabri za mitume waliopita ili kutoa mafundisho kwa watu lakini sio kama sira (biography) za mitume hao.

4.Injili 4 zilizomo kwenye Agano Jipya siyo injili zote zilizoandikwa. Zilikuwepo Injili nyengine nyingi, Ilifanyika Sinodi (Mkutano wa wawakilishi wa makanisa) mwaka 3225ili kuamua injili zipi zichukuliwe na zipi zikataliwe na hatimae injili ya Barnabas ilikataliwa. Na katilka historia ya kanisa viko vitabu vilivyokubaliwa na baadaye kukataliwa na kinyume chake. Ni binaadamu waliokuja badae ndio waliokuwa na uwezo wa kuamualipi lipi liwe neno la Mungu na lipi lisiwe. Katika uislamu hakukuwa na Ijitimai yoyote iliyokaa kuamua sura ipi iwe Qur-an ama isiwe.

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!