Ellimu Dini ya KiislamuNo Comments

Kutokana na umbile lake, mwanaadamu daima hutamani kuishi maisha ya furaha na amani yenye maana na yenye kufikia lengo, kwa hiyo kinadharia angelienda kufuata Dini (njia sahihi) itakayo muhakikishia kufikia lengo la kuumbwa kwake kwa furaha na amani. Dini sahihi itakayo muezesha mwanaadamu kuishi kwa furaha na amani katika maisha ya hapa duniani na huko akhera hainabudi kuwa na sifa zifuatazo;-

1.Dini sahihi ni lazima ieleze ukweli juu ya maumbile, Dini sahihi ni lazima itoe taarifa za ukweli juu ya mwanaadamu na maumbile   yote yaliyomzunguka. Imfahamishe mwanaadamu juu ya muumba wakena vyote vilivyomzunguka, imfahamishe lengo lake la maisha na lengo la kuwepo viumbe vyote vilivyomzunguka vilivyo hai na visivyo hai. Pia imfahamishe ni ipi nafasi yake au hadhi yake  hapa ulimwenguni nan i vipi ataweza kufikia lengo lake la maisha nakubakia katika hadhi yake na pia imfahamishe kwa usahihi ni ipi hatma yake baada ya maisha ya hapa duniani.

2.Kanuni na sharia zinazofuatwa na Dini sahihi ni lazima ziende sanjari na kanuni na sharia zinazofuatwa na maumbile yake, Dini sahihi ni lazima immundie mwanaadamu mwenendo wa maisha unaolingana na mwenendo unaofuatwa na maumbile yote ikiwa ni pamoja na mwili wake ili kwenda sambamba na maumbile yaliyo mzunguka na kuepukana na migogoro ya aina yoyote.

3.Dini sahihi ni lazima iwe na uwezo wa kutosheleza mahitaji yote ya mwanaadamu ya kimwili na kiroho (hisia), Dini sahihi pamoja na kumuelekeza mwanaadamu namna bora ya kuunawirisha mwili wake na kuuweka katika siha nzuri, haina budi pia kumuelekeza namna ya kutosheleza hisia zake. Dini sahihi ni lazima imuelekeze mwanaadamu kwa usahihi namna atakavyokabiliana na hali kama hizo na kubakia katika lengo lake.

4.Dini sahihi haina budi kuwa njia ya maisha iliyokamilika, Dini sahihi ni lazima umuwekee mwanaadamu utaratibu wa maisha utakaomuwezesha kukiendea kwa ufanisi kila kipengele cha maisha yake ya kibinafsi na kijamii katika Nyanja zote za kiafya, kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, kisheria na kielimu nakadhalika

5.Dini sahihi haina budi kuwa dini ya walimwengu wote wa nyakati zote, Binaadamu asili yao ni moja , lengo la maisha yao ni moja, na wote wanahitaji kuishi kwa furaha na amani. Hivyo dini sahihi haina budi kuwa dini inayowahusu waanadamu wote wa walimwengumzima kuanzia wa mwanzo mpaka wa mwisho, dini hiyohaina budi kutokuwa na mipaka ya jigrafia, siasa au wakati. Pia dini sahihi haitakuwa kwa jina la mtu, au la mahali au la kisheria.

6.Dini sahihi hainabudi kumuhakikishia mwanaadamu kupata haki zake zote, Dini sahihi inayowastahiki walimwengu wote wa nyakati zote hainabudi kuhakikisha kuwa mmoja anapata haki zake zote za kinafsi na kijamii bila ya upendeleo au ubaguzi wa ainayoyote . Dini, kabila, taifa,rangi, nasaba au hadhi havitazingatiwa na dini sahihi katika kumpatia kila mtu haki yake anayostahili. Pia dini sahihi hainabudi kuwa na sharia ambazo zinamgusa kila mtu kwa usawa.

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!