swahiliNo Comments

Jawabu.

Tamthiliya ni kazi ya fasihi iliyoandikwa kwa lengo la kuonyeshwa jukwaani, ambapo wahusika huzungumza na kutenda vitendo mbalimbali. Tamthiliya huigiza maisha ya kila siku.

Kwa kuwa tamthiliya imeandikwa kwa lengo la kuigizwa huwa imeandikwa na maelezo ya jukwaani, maelezo yanayoonesha nini kifanywe na nani na kwa namna gani.

Katika utunzi wa tamthiliya kuna mambo kadhaa ya kuzingatia, mambo hayo ni kama yafuatayo:

  • Chagua jambo unalotaka kuandikia
  • Panga namna msuko wa visa na matukioa utakavyokuwa
  • Buni wahusika wako kulingana na kile unachotaka kukiandika
  • Chagua mandhari yanayofaa kulingana na visa vyako
  • Tumia mtindo wa majibizano kati ya wahusika
  • Gawa tamthiliya katika maonyesho
    weka maelekezo ya jukwaa. Haya huelezea kile kinachotendeka kwa wakati ule. Maelezo ya jukwa huwa katika maandishi ya italiki.

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!