swahiliNo Comments

default thumbnail

Jawabu.

Shairi ni utungo wa kisanaa wenye mpangilio maalum wa lugha ya mkato unaowasilisha mawazo au ujumbe kuhusu mwanadamu au mazingira yake na hufuata utaratibu fulani. Uchambuzi wa mashairi una vipengele vifuatavyo:-

1. Anwani/kichwa cha shairi – Huwa ni muhtasari wa shairi katika neno au sentensi moja. Anwani ni kidokezo muhimu cha kinachozungumziwa katika shairi. Anwani huweza kuwa ya moja kwa moja, fumbo, kinaya, kibwagizo au sehemu ya kibwagizo. Ikiwa shairi halina anwani, basi lipewe anwani inayoafikiana na maudhui au dhamira kwasentensi isiyozidi maneno 6.

2. Maudhui – Haya ni masuala makuu au mambo muhimu yanayohusu mwanadamu au mazingira yake yanayozungumziwa katika shairi. Kwa mfano: malezi, siasa, usalama, unyanyasaji, ufisadi n.k. Maudhui hung’amuliwa kwa wepesi kutokana na kisa kilichomo katika shairi.

3. Dhamira / shabaha – Ni lengo kuu la mshairi katika kusanifu utungo wake. Dhamira ya mtunzi huwa ni ujumbe kwa kifupi anaoutambua msomaji kutokana na mwelekeo wa usemaji wa mtunzi katika shairi. Mfano: Baada ya kusoma shairi, unaweza kung’amua mtunzi alitaka kusisitiza kauli kuwa uongozi mbaya haufai, misitu ni uhai n.k. Dhamira hutokana na mwelekeo wa mawazo ya mshairi au falsafa yake.

4. Mbinu na tamathali za lugha – Ni mbinu za uandishi na tamathali za usemi zilizotumiwa na mshairi katika shairi. Mfano:Mazda / ziada / zidi – kurefusha maneno;enda kuwa enenda. Inksari

5. Muhtasari – Ni kufupisha maneno;aliyefika kuwa alofika. Utohozi – Mbinu ya kugeuza msamiati / maneno ya lugha geni ili yaandikike na kutamkika kana kwamba ni ya Kiswahili. Mfano: Time – taimu; One – Wani. Mbinu hii vilevile huitwa ukopaji au uswahilishaji.

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!