swahiliNo Comments

Jawabu.

Njia zote za uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi zina umuhimu mkubwa katika ukuzaji na uendelezaji wa utamaduni katika jamii. Kama ambavyo tumekwishaona, kazi za fasihi simulizi huelimisha, huburudisha, hurithisha maarifa, maadili, pia ni vielelezo vya utamaduni wetu wa asiili. Kwa ajili hiyo ni muhimu kuzihifadhi kazi hizo zisiharibike wala kupotea ili ziendelee kutumika kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

1. Kuhifadhi utamaduni; kazi za Fasihi ni muhimu ziendelee kuwepo ili kuhifadhi utamaduni wetu na huku vikitumika kama vivutio vya watalii.

2. Kazi za fasihi simulizi kwa upande mwingine ni sehemu ya ajira. Kwa mfano, shughuli mabalimbali za kisanaa kama vile ngoma, maigizo na utunzi wa vitabu, vinawapatia vipato baadhi ya wasanii. Hivyo ni muhimu zihifadhiwe.

3. Kazi za fasihi simulizi pia ni kichocheo cha umoja na maelewano miongoni mwa jamii. Yote hayo kwa ujumla wake yanabainisha kuwepo na haja ya kuendelea kuzikusanya, kuzifanyia kazi, kuziendeleza, na kuzihifadhi kazi za fasihi simulizi.

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!