swahiliNo Comments

Jawabu.

Wajerumani waliingia nchini Tanzania, baada ya ujio wa waarabu na wareno. Wajerumani walipoingia nchini Tanzania walikuta tayari Kiswahili kinatumika kwa kiasi Fulani. Ujio wao kama wakoloni, ulichangia sana kuenea kwa lugha ya Kiswahili. Njia zizotumika kueneza Kiswahili nchini Tanzania wakati wa utawala wa Wajerumani zilikuwa kama ifuatavyo:

(a)Utawala; Kutokana na ukweli kuwa lugha ya Kiswahili ilikuwa imekwisha kuenea, Wajerumani waliamua kutumialugha hiyo katika shughuli zao za ki-utawala.Wajerumani walilazimika kujifunza lugha ya Kiswahili huko huko Berlin kabla ya kuja nchini, kujifunza huko kulisaidia kuenea kwa Kiswahili. Kwa shughuli za kiutawala hapa nchini, ukolni wa Kijerumani ulitoa mwongozo kwa viongozi wa nchini kujifunza na kutumialugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano katika utawala. Hii ilimaanisha kwamba wajumbe na maakida wote iliwabidi wajifunze lugha ya Kiswahili ili wawe viungo wazuri wa serikali na wananchi.
(b) Elimu; Utawala wa Wajerumani uliteua lugha ya Kiswahili itumike kama lugha ya kufundishia, na pia kutumika kama somo la kawaida katika shule za msingi. Baadhi ya shule hizo ni kama vile Tabora, Mpwapwa na Kilosa,kwa mtazamo huo, wanafunzi na walimu walijifunza Kiswahili ili wakitumia katika shughuli za elimu na hivyo kufanya lugha hiyo kuenea kwa urahisi.

(c) Shughuli za kilimo (Mashamba); Moja ya shughuli walizofanya Wajerumani, ilikuwa kuanzisha mashamba makubwa ya mazao ya biashara kama vile katani huko Tanga na kahawa huku Kilimanjaro na Bukoba. Katika mashamba haya kulikuwa na idadi kubwa ya vibarua kutoka sehemu mbalimbali za nchi,lugha iliyotumika ni Kiswahili, ambacho kilitumiwa na vibarua hao. Hivyo Kiswahili kilikuwa na ongezeko la watumiaji na kufanya lugha hiyo kuenea.

(d) Mahakama; Utawala wa Kijerumani ulitumia pia lugha ya Kiswahili katika shughuli za kimahakama. Wafanyakzai na wazee wa mahakama waliwahoji na kutoa hukumu kwa watuhumiwa kwa kutumialugha ya Kiswahili. Hivyo shughuli za kati ziliendeshwa kwa Kiswahili na kufanya kiswaili kienee chini ya utawala huu.

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!