swahiliNo Comments

Jawabu.

Kukua kwa lugha ni hali ya kuongezeka kwa msamiati wa lugha hiyo. Msamiati ni jumla ya maneno yanayotumiwa katika lugha Fulani, ili lugha yoyote ikuwe lazima msamiati wake ukuwe.

Wageni wa kwanza kuja Tanzania ni waarabu,kutokana na kuhusiana na waarabu katika Nyanja mbalimbali. Ksiwahili kimechukua msamiati wa kiarabu ili kukuza msamiati wake, ni tabia ya lugha zinapotumika pamoja huathiriana na kuchukuliana maneno.

Yasemakana kiingereza kimeathiriwa na kilatini kwa kiasi cha theluthi mbili. Kiswahili kimeathiriwa na lugha nyengine kama vile kihindi, kiajemi, kireno, Kijerumani, Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu n.k. Kiarabu ndicho chenye maneno mengi sana katika Kiswahili kuliko lugha ya taifa lolote jengine la kigeni, hii ni kwa sababu zifuatazo;

(a)Bara Arabu ndiyo nchi ya kigeni iliyokuwa jirani zaidi na upwa wa Afrika Mashariki, hivyo watu wake waliingiliana zaidi na watu wa huku kuliko watu wengine wowote, maingiliano hayo hayakuwa ya kibiashara tu bali hata ya kindoa.

(b) Lugha ya kiarabu ndiyo lugha iliyotumika kufundishia dini ya kiislamu, hivyo waswahili walijikuta wanaingiza maneno ya kiarabu katika Kiswahili. Zifuatazo ni sababu zilizopelekea ukuaji wa kiswahili wakati wa waarabu:-

1.Dini: Waarabu walipowasili walianza kueneza dini yao ya kiislam kwa wenyeji wa upwa wa Afrika. Waarabu walianzisha madarasa ambayo walitumia kufundishia waafrika dini ya kiislam, wafrika hao walifundishwa kusoma na kuandika kwa hati za kiarabu ili waweza kusoma na kuelewa Qur-an. Lugha ya kufundishia katika madarasa hayo ilikuwa Kiswahili, hivyo waswahili walijikuta wanaingiza baadhi ya maneno katika Kiswahili. Kutokana na dini na elimu tumeweza kupata maneno ambayo tunatumia katika Kiswahili, maneno hayo ni kama vile; alajiri, alasiri, kurani, elimu, ratibu, inshallahn.k

2. Utawala: Kutokana na kutawaliwa na waarabu,tumepata msamiati mwingi wa Kiswahili. Waarabu walitawala Pemba, Unguja na sehemu za pwani za bara. Kutokana na kutawaliwa kuna baadhi ya maneno ambayo yamechukuliwa kutoka lugha yakiarabu na kuwa katika Kiswahili,maneno hayo ni kama vile sultani, mwinyi,utukufu, enzi n.k

3. Biashara: Waarabu walipowasili katika mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki, walianza kufanya biashara na wenyeji,kutokana na maingiliano hayo ya kibiashara , waarabu walianza kuingiza maneno mengi ya kiarabu katika lugha ya Kiswahili. Kutokana na maingiliano hayo ya kibiashara, Kiswahili kilianza kupanuka kwakuongeza msamiati, na bila shaka hali hii ilisababihsa kukuwa kwa Kiswahili,mfano wa msamiati uliochukuliwa kutoka kwa waarabu na kingizwa katika Kiswahili ni jahazi, kodi, adesi n.k.

4. Waarabu na ndo za wabantu: wageni hawa walikaa kwa miaka mingi sana katika pwani ya Afrika Mashariki, walijikuta walowezi ambao milazao na Kiswahili zilianza kuchangamana kwa kiasi fulani. Hivyo, waarabu walijikuta wanatwa wake wa kibantu ili waishi kama mume na mke,lugha ambayo ilitumika sana katika maisha yao ya ndo ilikuwa ni Kiswahili.
Vile vile watoto waliozaliwa na wazazi wa kiarabu na kibantu walijifunza Kiswahili na kukitumia kamalugha yao ya awali.malezi ya watoto hawa yaliegemea kwenye utamaduni wa Kiswahili, watoto hawa walikuzwa kwa lugha ya Kiswahili. Hata jamii ya watu wa pwani na Tanzania kwa ujumla waliwaita watoto hawa “Waswahili” baada ya maneno kama vile “Chotara”. Kwa ujumla utaona ndoa za waarabu na wabantu zilichangia pia katika kueneza lugha ya Kiswahili hapa nchini Tanzania.

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!