swahiliNo Comments

Lugha ni sauti za nasibu zenye kuleta maana ambazo zimekubaliwa na wanajamii kutumika kwa mawasiliano miongoni mwao. Kulingana na tafsiri hii , tunabaini kwamba, sifa mojawapo ya lugha ni kutoa maana ambayo inaeleweka kwa watumiaji wake.Kinyume na hivyo haiwezi kuwa lugha. Ndiyo sababu milio ya viumbe, kama vile wanyama, ndege, na wadudu siyo lugha kwa vile hazitoi maana. Kwa hiyo kama tusingekuwa na lugha wanaadam tusingeweza kuwasiliana kwa maana tunavyofanya sasa. Lugha ina dhima kubwa katika mawasiliano ndani ya jamii zetu kama vile:

1. Lugha ni utambulisho wa jamii: Lugha ikiwa kama nyezo kuu ya mawasiliano, vilvile ni kitambulisho mahsusi kwa watumiaji wake. Kwa kuwasikia watu wanazungumza lugha Fulani, tunapata kuwafahamu watu hawa ni wa jamii gani.

2. Lugha hutumika kama nyenzo ya kudhihirisha hisia: Kupitia lugha, wanaadamu huweza kudhihirihisha hisia, kama vile upendo, wasiwasi, chuki, simanzi, woga, ukaili n.k.

3. Lugha ni seheu ya utamaduni wa watu: Lugha hubeba jukumu la kudumisha utamaduni. Vizazi hurithishwa mila, desturi na amali za jamii kupitia lugha.

4. Lugha huelimisha: Watu hujifunza na kupata maarifa, stadi, mielekeo na maadili shuleni au popote pale kupitia lugha. Ingawa lugha ni kiungo muhumu sana katika maisha ya binaadam, huweza kuwa na athari hasi, hali hii hutokea pale lugha inapotumiwa kuwachonganisha watu au kueneza chuki na uhasama.

5. Lugha fasaha na Umuhimu wake: Ufasaha ni utamkaji wa maneno ya lugha kwa usahihi na kuyapa maana kamili na sahihi. Katika mazungumzo na maandishi, ufasaha hutokana na mpangilio wa maneno na miundo mbinu ya sentensi unaowasilisha kwa usahihi.

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!