swahiliNo Comments

Jawabu.

Tungo tata ni tungo ambazo huwa na maana zaidi ya moja ndani yake. Mara nyingi utata katika lugha ya kiswahili hujitokeza katika maandishi kuliko kwenye mazungumzo kwa sababu mazungumzo huzingatia zaidi mazingira ya wazungumzaji na wakati.

(a) Kutoa maana zaidi kwa yale maneno yenye maana zaidi ya moja na kuongeza viambishi ili kubainisha maana iliokusudiwa. Kwa Mfano Mbuzi wake ameibiwa au Mbuzi wake wameibiwa

(b) Kuzingatia kanuni za uandishi hasa ni matumizi na alama na vituo tunapoandika. Mfano (i) Mama latifa yupo? (ii) Mama, latifa yupo. (iii) Mama, latifa yupo? (iv) Mama latifa yupo.

(c) Kuzingatia matumizi sahihi katika mazingira muafaka ya vinganishi na vihusishi. Kwa Mfano Ali anakula wali kwa kuku baala ya Ali anakula wali na kuku

(d) Tueke shada au mkwazo kwa yale maneno yanayohitaji hali hiyo, ili kupata maana iliyokusudiwa. Kwa mfano Ali ameonekana barabara

(e) Tuyaepuke matumizi mabaya ya fasihi, kwa sehemu zisizo hitajika yaani tutmie lugha ya kawaida. Kwa Mfano Baada ya kusema Ali amevaa miwani basi tuseme Ali amelewa.

(f) Tueke bayana matumizi ya vitendo kwa kutoa maelezo zaidi kwa vile vitendo vinavyotoa maana zaidi ya moja tunapotumia katika tungo. Kwa mfano Baada ya kusema mtoto wake ameibiwa basi tuseme Vitu vya mtoto wake vimeibiwa.

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!