swahiliNo Comments

Jawabu.

Kisakale ni hadithi inayohusu matukio yaliyowahi kutokea zamani. M.M. Mulokozi anasema visakale ni masimulizi ya kimapokeo juu ya wahenga na mashujaa wa kabila au taifa yenye kuchanganya chuku na historia. Aghalabu kadhia zinazosimuliwa kwenye visakale ni kama vile njaa, kiangazi, magonjwa ya kuambukiza, uhamaji na vita.

Wahusika wengi wa visakale ni binadamu wenye uwezo mkubwa au mdogo kutegemeana na mantiki wanayowekewa. Visakale hufananishwa sana na tendi kwa sababu vyote kwa pamoja huhusu masimulizi ya kishujaa.

Mfano wa kisakale ni: Kisa cha Liyongo ambacho kinashabihiana sana na utendi wa Fumo Liyongo kwa kuwa vyote huzungumzia ushujaa. Tofauti kubwa ni kuwa kisakale cha Liyongo ni utanzu wa kinathari na utendi wa Fumo Liyongo ni utanzu wa kinudhumu (kishairi).

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!