swahiliNo Comments

Jawabu.

Tungo tata ni tungo ambazo huwa na maana zaidi ya moja ndani yake. Mara nyingi utata katika lugha ya kiswahili hujitokeza katika maandishi kuliko kwenye mazungumzo kwa sababu mazungumzo huzingatia zaidi mazingira ya wazungumzaji na wakati. Zifuatazo ni sababu za utata katika lugha ya Kiswahili:-

(a) Msamiati kuwa na maana ya zaidi ya moja, Hii ni sababu kuu inayo onesha utata katika lugha ya kiswahili . Neno moja kuweza kutumika na kutoa maana kadhaa. Kwa Mfano Pamba, mbuzi, taa, kaa, mezam tupa, onyesha, Buni, shinda nk haya yote ni maneno yanayo sababisha utata na kuwa na maana zaidi ya moja.

(b) Kutozingatia taratibu za uandishi, hii ni kukiuka matumizi ya sahihi ya vituo na alama au kutumia vibaya pia kuna sababisha utata katika tungo. Kwa Mfano katika sentensi hii tunweza kupata maana zaidi ya moja;- Mama, latifa yupo?, Mama latifa yupo?, Mama, latifa yupo au Mama latifa yupo.

(c) Matumizi yasiyokuwa bayana ya viunganishi au vihusishi; Tunapotumia viunganishi au vihusishi kimakosa basi huweza kuleta utata katika tungo. Kwa Mfano Ali anakula wali na kuku na Biharusi ameletwa na gari.

(d) kukosekana kwa shada au mkwazo kwa baadhi ya maneno, Pia husababisha utata katika lugha mfano neno barabara linapowekwa mkwazo huleta maana tafauti na kama halijawekwa mkwazo kuleta maana tafouti.

(e) Matumizi ya fasihi, Pia matumizi ya fasihi husababisha utata kwani maana ya mzungumzaji huwa ni kinyume na ile ya kawaida. Kwa Mfano Ali amevaa miwani na Mzee Ali mfano la chumvi nyingi.
(f) Kutokuonesha wazi kitu kinamuhusu nani katika tungo, Tungo haiwezi kubainisha wazi kitu kilichokusudiwa .Mfano Hutoka alfajir na mbwa wake ili apate afanye mazoezi

Be the first to post a comment.

Add a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

error: Content is protected !!